Mwandishi Mkongwe wa Habari za Michezo nchini, Willie Chiwango (61) amefariki dunia.

Taarifa kutoka mtoto wa marehemu, Stephen Chiwango, zinasema mauti ya limfika baba yao jana saa 5:30 usiku katika hospitali ya Masana iliyopo Mbezi Beach jijini Dar es Salaam alikokua amelazwa kwa matibabu na alikua akisumbuliwa na matatizo ya kichwa.

Alisema kuwa mauti yalimkuta katika hospitalini hapo akifanyiwa vipimo zaidi ili kujua tatizo la mwandishi huyo ambaye chombo chake cha mwisho kukifanyia kazi ni Tanzania Standard Newspapers (TSN) akiwa ni Mhariri Msanifu wa Michezo Gazeti la Daily News.

Alisema kuwa mwili wa Chiwango bado uko Masana na ndugu wanafanya mipango ili kwenda kuuhifadhi katika chumba cha kuhifadhia mahiti cha hospitali ya Lugalo, Mwananyamala au Amana.

Alisema baada ya kuuhifadhi mwili wa mpendwa wao, ndugu watakutana kwa ajili ya mazungumzo ili kujua mazishi yatafanyika lini na wapi.

Marehemu Chiwango ameacha mke na watoto wawili.
Tulimpenda Chiwango, lakini Mungu Amempenda Zaidi!

Mroki Mroki at Friday, December 04, 2015
CHANZO CHA HABARI HII: mrokim.blogspot.com

Azam FC Waiumiza Kichwa Kambi Ya Simba SC
Tanzania Yajikongoja Viwango Vya Ubora Duniani