Mwandishi wa idhaa ya Idhaa ya Kiswahili ya Deutsche Welle (DW) , Salma Said, aliyekuwa amepotea katika mazingira ya kutatanisha tangu Machi 18 mwaka huu, amepatikana jana jijini Dar es Salaam.

Taarifa za kupatikana kwa Mtangazaji huyo zimethibitishwa na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon Siro pamoja na DW kupitia ukurasa wao wa Facebook.

Mume wa Salma anayefahamika kwa jina la Ali Salim Khamis aliiambia BBC kuwa mkewe amepatikana na yuko chini ya Jeshi la Polisi jijini Dar es Salaam akitoa maelezo ya mkasa uliomkuta.

Awali Jeshi la Polisi lilisema kuwa halina taarifa juu ya kukamatwa kwake, hali iliyozua taharuki zaidi.

Louis van Gaal: Rashford Ni Shujaa Wa Man Utd
Maalim Seif afunguka wakati wazanzibar wakipiga kura, ‘nasubiri rais atangazwe’