Mwandishi wa Habari wa shirika la utangazaji la Taifa la Kongo, RTNC Heritier Magayane ameripotiwa kuuawa baada ya kupokea simu kutoka kwa mtu asiyejulikana.

Maofisa wa mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wamesema kuwa mwandishi huyo ameuawa kaskazini mwa jimbo la Kivu.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na mfanyakazi mwenzake ambaye waliwahi kufanya kazi pamoja Roger Sebyeradu, amesema mauaji ya mwandishi huyo yanaweza kuwa na uhusiano na kazi yake, baada ya kutangaza kipindi ambacho aliwataka vijana kuhamasisha amani.

Sebyeradu amesema kuwa mwandishi huyo alipokea simu ya mtu ambaye alikuwa anataka kukutana naye katika kijiji cha Bunyangula ambapo aliuawa.

Jeshi la Rwanda lavunja ngome ya 'Al-Shabaab' Msumbiji
Rais Mwinyi akutana na Kamishna Mkuu TRA