Watu watatu, Mfungwa pamoja na mahabusu waliokuwa katika gereza la Butimba jijini Mwanza, wameuawa mmoja kwa risasi na wengine kwa kupigwa na wananchi waliotoa usadizi kwa askari kuwakamata baada ya kutoroka gerezani.
Kamanda wa polisi wa mkoa, Jumanne Muliro amesema tukio hilo lilitokea Aprili 14 mwaka huu saa 12: 30 jioni katika gareza kuu la mkoa wa Mwanza la Butimba.
Amesema watuhumiwa hao ni mahabusu namba 3444/2016 Yusuph Bernard (34), seleman seif (28) mwenye namba 1177/2017 mwenye kesi ya mauaji.
Mtuhumiwa wa tatu amesema ni mfungwa namba 200/ 2019 aliyekuwa amefungwa miaka 15 kwa kosa la uhujumu uchumi, George Aloyce (34) lakini pia alikuwa na kifungo kingine cha kutoroka chini ya ulinzi kwa miezi sita.
Kamanda Muliro amesema watuhumiwa hao baada ya kutoroka, askari magareza kwa kushirikiana na wananchi waliwafukuza na kufanikiwa kuwakamata ambapo wananchi waliwashambulia kwa kipigo katika sehemu za miili yao na kusababisha hali zao kuwa mbaya.
” Baadaye walipelekwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa ya Sekou Toure kwaajili ya matibabu, lakini ilipofika jioni walifariki dunia wakati wakipatiwa matibabu” Amsema Kamanda huyo