Muasisi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Mzee Edwin Mtei amemsifu rais John Magufuli kwa kazi yake ikiwa ni muda mfupi tangu aingie madarakani.

Mzee Mtei ambaye pia ni Gavana wa kwanza wa Benki Kuu ya Tanzania, amesema kuwa rais Magufuli ni mtu ambaye anaonesha shauku ya maendeleo.

Aliongeza kuwa endapo rais Magufuli ataendelea kuishi kile anachokisema, anaamini atasimamia vizuri ukuaji wa uchumi wa nchi.

Hata hivyo, mzee Mtei alieleza kuwa rais Magufuli anachofanya hivi sasa kwa kiasi kikubwa anatekeleza ilani ya Chadema.

“Kile anachofanya kwa sasa kimekuwa ni kilio cha muda mrefu kwenye ilani na sera zetu na tutashirikiana naye kumsaidia kuendeleza nchi hii, “Mzee Mtei aliiambia Mwananchi katika mahojiano maalum.

Alimshauri rais Magufuli kuhakikisha kuwa uwekezaji unaofanywa na wageni unawafaidisha zaidi wananchi tofauti na ilivyokuwa awali.

” Nashauri wageni wanaotaka kuwekeza katika sekta ya madini, wauze hisa zao kwa serikali ambayo itakuwa ikimiliki hisa nyingi zaidi. Kwa kufanya hivyo, maliasili za nchi zitawanufaisha wananchi,”alisema.

Masaburi Abariki Ubunge wa Kubenea, atakiwa Amlipe Fidia
Viongozi Wa Chelsea Wakutana Kumjadili Mourinho