Mwanzilishi na mmiliki wa mtandao wa Facebook, Mark Zuckerberg ametangaza kuwapa masikini asilimia 99 ya hisa zake katika mtandao huo baada ya kumpata mtoto wake wa kike aitwae Max.

Zuckerberg ametumia furaha aliyonayo kwa kumpata mtoto huyo wa kike alizaa na mkewe ambaye ni daktari, Priscilla Chan kutoa asilimia hizo za hisa ambazo ni zaidi ya $45 bilioni kwa ajili ya kuwasaidia masikini.

Wawili hao waliandika ujumbe huo kupitia barua kwa mtoto wao huyo,

Zuckerberg na Chan ambao wameanzisha shirika lisilo la kiserikali linaloitwa ‘Chan Zuckerberg family’ lenye lengo la kusaidia masikini kwa kuwapa huduma za elimu na afya, wameeleza kuwa wataendelea kufanya hivyo kwa muda wote wa maisha yao.

“We will give 99% of our Facebook shares — currently about $45 billion — during our lives to advance this mission,’ ‘We know this is a small contribution compared to all the resources and talents of those already working on these issues. But we want to do what we can, working alongside many others.We’ll share more details in the coming months once we settle into our new family rhythm and return from our maternity and paternity leaves. We understand you’ll have many questions about why and how we’re doing this.” Inasomeka sehemu ya barua hiyo.

Jipange: Kutupa Taka Hovyo faini 50,000, Watakaosaidia Kukamata Kuzawadiwa
Patoranking Anatafuta Mwanamke Wa Kuoa, Aelezea Sifa Zake