Hatimae Ripoti ya kilimo barani Afrika ya mwaka 2020 imezinduliwa kwenye Mkutano wa kilele wa mapinduzi ya kijani Afrika (AGRF) jijini Kigali,Rwanda .
Uzinduzi wa ripoti hiyo ambayo ni toleo la 10 umewaleta pamoja wadau 4,000 ,ikiwa ni pamoja na wakuu wa nchi na serikali ,mawziri wa kilimo ,washirika wa asasi za kijamii ,viongozi sekta binafsi ,wanasayansi na wakulima ili kujadili namna ya kuzalisha chakula cha kutosha kwa kuzingatia ongezeko la watu mijini.
Hii ni mara ya kwanza kwenye historia ya baraza la kilimo Afrika kukutana ikiwa bara hili linachangamoto ya ugonjwa wa Covid-19 .
Kauli mbiu ya mwaka huu “lisha jiji,kuza bara: kutumia soko la chakula mjini kupata mfumo wa chakula endelevu Afrika” .
Ripoti imejikita zaidi katika kulisha majiji na miji kwa kutumia fursa ,changamoto na sera zinazowezesha wakulima wa kiafrika kufaidika na ukuaji wa soko la chakula mijini .
Moja ya lengo la ripoti hii ni kutafuta njia kwa wakulima wadogo kuweza kulinda chakula kupata ustawi vijijini na kukuza uchumi wa pamoja.
“ripoti inaangazia fursa kwa weadau wote wa kilimo kuja pamoja kuchambua ajenda ya mabadiliko , pia kupiga hatua kiutendaji kwenda kwenye mapinduzi ya kilimo” amesema Dokta Agness Kalibata rais wa muungano wa mapinduzi ya kijani wakati wa uzinduzi wa ripoti .
Ripoti imeanza kwa kuangazia soko la chakula mijini kwa wakulima milioni 60 barani Afrika na ushiriki wa taasisi mbalimbali katika ukuzaji wa kilimo na upatikanaji wa chakula .