Winga wa Yanga, Geofrey Mwashiuya, amesema kuwa Klabu ya Simba imemfuata ikitaka asaini kuichezea timu hiyo.

Pamoja na Simba, Mwashiuya pia ameeleza kuwa Kocha wa Azam FC, Aristica Cioaba, raia wa Romania, naye anamtaka

Timu hizo zimemfuata Mwashiuya wakati akiwa amebakiza mkataba wa miezi sita na klabu yake hiyo inayonolewa na Mzambia, George Lwandamina ambayo juzi Jumamosi ilibanwa mbavu na kupata sare ya bao 1-1 dhidi ya Prisons.

Mwashiuya amesema kuwa kweli Azam na Simba wamekuwa wakimmendea kwa ajili ya kumsajili ambapo hadi sasa viongozi wa timu hizo wameshamfuata kwa ajili ya kumalizana naye.

“Ni kweli kwamba viongozi wa Azam wamekuja kwa ajili ya kuongea na mimi, wakiwa wanataka wanisajili kwenda kuongeza nguvu kwenye klabu yao wakisubiri muda wangu umalizike ili wanichukue.

“Kwa sasa nimebakisha mkataba wa miezi sita hapa Yanga, lakini ukiondoa Azam hata Simba nao wamekuja kuzungumza kwa ajili ya kunisajili,” alisema winga huyo ambaye alitokea Kimondo FC ya Mbeya kabla ya kutua Yanga.

Chanzo: Gazeti la Champion

Serikali kugawa Kondomu bure
Waamuzi 18 Tanzania wapata beji FIFA 2017/18