Boniface Gideon, Pangani.

Chuo  cha Usimamizi wa Wananyamapori Mweka cha mkoani Kilimanjaro,  kimetoa msaada  kwenye Kituo cha kulea Watoto Yatima cha Micapi Village pamoja  na familia yenye Walemavu 14.

Msaada huo wa Chakula na bidhaa za usafi, ni sehemu ya utaratibu wa Chuo hicho katika kurudisha shukrani kwa jamii, ambayo ilitolewa kwa wahitaji hao katika Shule ya Msingi Funguni, iliyopo Wilayani Pangani Mkoani Tanga.

Akikabidhi msaada huo, Naibu Mkuu wa Chuo hicho Prof. Wahabu Kimaro amesema  jamii zinazopitia katika changamoto huwa wanaziangalia kwa karibu na wanazitembelea kuwasaidia mahitaji mbalimbali.

“Taarifa za familia yenye watoto wanane na wajukuu ambao huzaliwa wakiwa walemavu tulizipata kupitia kwa Afisa Ustawi wa Jamii wa Wilaya ya Pangani,” alisema Prof. Kimaro

Kwa upande wake Afisa Ustawi wa Jamii Wilaya ya Pangani, Said Kileo amewaomba wadau kujitokeza na kuzisaidia familia hizo zinazokabiliwa na changamoto za ulemavu.

Daktari Mtibwa Sugar afunguka hali ya Makaka
Simba yaichorea ramani Coastal Union