Uwekezaji wa Pauni Bilioni 1.57 wa Bilionea Jim Ratcliffe kwenye klabu ya Manchester United unatarajiwa kuthibitishwa kuanzia Juma lijalo na mchakato wake unaweza kukamilika Jumatatu.

Ratcliffe, Bilionea wa pili wa Uingereza anayekadiriwa kuwa na utajiri wenye thamani ya Pauni Bilioni 29.6 amefikia makubaliano ya kununua asilimia 25 za hisa kutoka kwa familia ya Glazer ambaye ni mmiliki wa klabu hiyo kwa sasa.

Huku wana familia wa Bryan, Edward, Kevin na Darcie, wote wameorodheshwa kama wakurugenzi wa klabu ya Man United wanatarajia kupunguza hisa zao kwa kiasi kikubwa kama sehemu ya mauzo ya klabu hiyo huku wenyeviti Avram na Joel Glazer watabaki na wataendelea na umiliki mkubwa katika familia ya Glazers.

Lakini Ratcliffe, muasisi wa kampuni ya kemikali ya Ineos atakuwa na utawala wa uendeshaji wa soka katika klabu hiyo katika mpango wa kurejesha mafanikio ya timu iliyofanikiwa zaidi katika historia ya Ligi Kuu ya England na ambao mara ya mwisho kushinda ubingwa wa ligi ilikuwa mwaka 2013.

ESPN iliarifu mapema msimu huu kwamba timu ya Ratcliffe tayari imeanza kufanya ukaguzi wa mahesabu kuzuia upotevu mkubwa wa fedha kwenye usajili wa wachezaji kama ambavyo imetokea chini ya Glazer.

Lakini pamoja na kufikia makubaliano ya kununua asilimia 25 za hisa kwenye klabu hiyo miezi miwili iliyopita, mazungumzo na familia ya Glazers yanaenda taratibu na Richard Arnold ameacha kazi yake kama mtendaji mkuu kwenye mchakato huo.

Zanzibar kunufaika ufadhili wa masomo Uturuki
Simba SC yaahidi kupambana Morocco