Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa amesema ujenzi wa miundombinu ya barabara nchini unafanyika kwa umakini na viwango vya ubora chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Waziri Bashungwa ameyasema hayo hii leo Septemba 20, 2023 akiwa Ikwiriri Mkoani Pwani, ikiwa ni mwendelezo wa ziara ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa Mikoa ya Kusini.

Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa.

Amesema, “kazi yetu ni kutekeleza yale ambayo Rais ametuagiza, kwenye maelekezo uliyotupatia ya utiaji saini mikataba mbalimbali ambayo inakaribia trilioni 2 hata TARURA watakuwepo kuonesha namna Serikali yako ilivyojipanga katika ujenzi wa barabara.”

Aidha, Waziri Bashungwa pia amesema Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameagiza upembuzi yakinifu wa ujenzi wa Barabara ya Mabasi yaendayo haraka kutoka Mbagala kuelekea Vikindu ufanyike haraka, ili utaratibu wa kuanza ujenzi uanze.

Supercomputer yairudisha Chelsea Ulaya
Khamis atupwa Jela miaka 20 kwa shambulio la aibu