Leo Oktoba 7, 2023 Mkuu wa Mkoa Dodoma, Rosemary Senyamule amekabidhi Mwenge wa Uhuru kwa Mkuu wa Mkoa Manyara, Queen Sendiga.

Makabidhiano hayo yamefanyika katika Wilaya ya Kiteto, huku Senyamule akisema Mwenge huo wa uhuru ukiwa Mkoani Dodoma umekusanya chupa 209 za Damu, ambazo zitawasaidia watu wenye uhitaji maalum, wakiwemo kina mama wajawazito.

Mkuu wa Mkoa manyara, Queen Sendiga.

Naye Mkuu wa Mkoa manyara, Queen Sendiga amesema mwenge huo utakimbizwa na kukagua miradi 58 yenye thamani ya shilingi 13.4 Bilioni na utakimbizwa katika Wilaya zote za Mkoa.

Mbio hizo zitahitimishwa Oktoba 14, 2023 katika uwanja wa Tanzanite Mjini Babati ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania, Dkt. Samia suluhu Hassan.

Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Oktoba 8, 2023
Tisa wahukumiwa kunyongwa kwa mauaji Njombe