Massimiliano Allegri sasa rasmi atachukua nafasi ya Andrea Pirlo kama meneja wa Juventus baada ya kuipiga chini Real Madrid dakika za mwishoni mwishoni kabisa..

Makubaliano yamefikiwa kwa Allegri kurudi Turin, na kocha huyo mwenye umri wa miaka 53 alikuwa ameondoka ndani ya klabu hiyo mnamo 2019 na nafasi kuchukuliwa na Maurizio Sarri ambaye nae alitimuljwa Majadiliano kati ya mwenyekiti wa Juve, Andrea Agnelli na Allegri yamefikia hitimisho vizuri, na Pirlo ameamua kuachia nafasi yake kama mkufunzi mkuu kufuatia msimu mbovu wa 2020-21 ambao walikuwa wakipambana kumaliza nne bora na Ubingwa kuukosa mapema tu.

Juventus wamefikia makubaliano na Allegri baada ya kufungua tena mazungumzo katika siku chache zilizopita Allegri alikuwa akiwasiliana moja kwa moja na bodi ya Real Madrid tangu Machi na alikuwa Anasubiri kazi ya Real kwa miezi sasa ndipo akaamua kujiunga na Juventus kwa sababu ya Florentino Perez kuchukua ‘muda mrefu sana’ kumteua pia baada ya Zinedine Zidane kuamua kuondoka klabuni.

Inter pia walikuwa wakijaribu kumshawishi Allegri lakini rais wa Juventus Andrea Agnelli aliamua kuboresha ofa yake ya kumnasa Allegri mara moja ambaye Baada ya kujiunga na Juventus mnamo 2014, alishinda mara nne mfululizo mataji ya ndani kati ya 2015 na 2018, kocha pekee aliyefanikiwa kufanya hivyo katika ligi tano bora za Ulaya; Allegri aliondoka Juventus na asilimia ya ushindi wa 70.48%, ambayo kwa sasa ni ya juu zaidi katika historia ya Juventus pia alipoteza fainali mbili za Ligi ya Mabingwa Ulaya alizofika na Vibibi hivyo vya Turin.

Kiongozi wa mapinduzi ya Mali ajitangaza Rais, awavua madaraka Rais, Waziri Mkuu
Jaji Warioba: Ajira za Serikalini hazitoshi