Mwenyekiti wa Kamati ya Mazingira wilayani Kiteto mkoani Manyara, Engerusi Mikonde (59), ameuawa katika shambani akiwa kwenye harakati za kutatua mgogoro wa ardhi baina ya wakulima na wafugaji.

Kamanda wa Polisi mkoani humo, Augostino Senga amethibitisha kutokea kwa tukio hilo akisema uchunguzi unaendelea na kwamba mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya wilaya Kiteto.

Mmoja wa shuhusa wa tukio hilo Daiomoni Nzungu, amesema Mikonde akiwa na kamati ya mazingira kutafuta ufumbuzi wa mgogoro wa wakulima Kijijini hapo, alishambuliwa kwa marungu na mapanga hadi alipokutwa na umauti.

Waziri asisitiza elimu matumizi ya gesi

Baadhi ya wananchi wamelitaka jeshi la polisi kufanya uchunguzi wa kina juu ya tukio hilo wakisema kuwa suluhu ya sakata hilo ni kupatikana kwa taarifa ya kina ili sheria ifuate mkondo wake kwa waliohusika.

Migogoro mingi ya wakulima na wafugaji wilayani Kiteto huanza kipindi ambacho wakulima wanaandaa mashamba huku wafugaji wakihitaji maeneo kwaajili ya shughuli za kufugia mifugo yao.

Mbunge aponda mvuto wa wahudumu ndege za ATCL
Samatta amchambua 'fundi aliyempikia' bao la kuifunga Liverpool