Mwenyekiti wa Chama Cha Walimu (CWT) Wilaya ya Chato, Lucas Michael maarufu kama Masai, aliyepanda kwenye jukwaani katika mkutano wa mgombea urais kupitia Chadema, Edward Lowassa.

Mwenyekiti huyo alipanda jukwaani Septemba 19 katika jimbo la Chato na kuueleza matatizo ya Walimu katika wilaya hiyo ambapo alidai kuwa serikali ilishindwa kuwasafirisha walimu, kuwalipa fedha za masomo, pamoja na kuwakandamiza walimu ambao walionekana kuwa upande wa upinzani katika wilaya hiyo huku wale ambao walionekana kuisapoti CCM wakionekana wako sahihi.

Mwenyekiti huyo ameshitakiwa kwenye Tume ya Utumishi wa Umma Idara ya Utumishi wa Walimu wilayani hapo kwa madai ya kwenda kinyume na Kanuni za maadili na taratibu za utumishi namba 65 (1). Katika hati ya mashtaka iliyosainiwa na Kaimu Katibu wa Tume ya Utumishi wa Umma, Frank Angus, Mwenyekiti huyo anadaiwa kukiuka sheria ya utumishi wa umma kwa kujihusisha na masula ya siasa, kutoa taarifa za kiutumishi kwenye mikutano ya kisiasa pamoja na kutumia cheo chake kumnadi mgombea urais, hivyo anapaswa kujitetea mbele ya Tume hiyo.

Hata hivyo, Mwenyekiti huyo wa walimu alifanya mahojianona gazeti la Nipashe na kueleza kuwa yeye hakumpigia kampeni mgombea urais wa Chadema, bali alizungumzia malalamiko ya walimu wilayani humo kwa kuwa alipewa mualiko na uongozi wa Chadema kwa barua ambayo aliitaja kumbukumbu namba.

Liverpool Yaonyesha Dhahir Mapenzi Kwa Klopp
Lowassa: Mlitaka nife… Tupo na Tupo Hai