Aliyekuwa mwenyekiti klabu ya Simba, Swedi Mkwabi ameamua kujiuzulu nafasi hiyo kwa kile alichodai kuwa anahitaji muda zaidi ili kusimamia shughuli zake binafsi.

Taarifa hiyo imetolewa mapema leo Septemba 14, 2019 na uongozi wa klabu ya Simba kwa wanachama, mashabiki na wananchi wote.

Swedi aliamua kuiandikia barua Bodi ya Wakurugenzi kupitia Mwenyekiti wa Bodi akitoa taarifa hiyo ya kujiuzulu kwake.

Hivyo Bodi ya Wakurugenzi na Sekretarieti ya Simba baada ya kupokea taarifa hiyo imemtakia kila la heri, Swedi katika shughuli zake anazokwenda kuzisimamia.

Pia Bodi imesema itaendelea kushirikiana nae katika shughuli mbalimbali za klabu kama ilivyokuwa awali kabla kupata nafasi hiyo.

Mkwabi na mwekezaji Mo Dewji kwa muda sasa wamekuwa hawaelewani kiasi ambacho kinapelekea sintofahamu ndani ya Simba.

Inaelezwa kuwa Mo Dewji alikuwa hana Imani na Mkwabi kutokana kuonekana kuwapa nguvu kundi linalompinga likiongozwa na Mzee Kilomoni , Mo anaamini Mkwabi anavujisha Siri za vikao ndani ya Simba kwa kina Mzee Kilomoni kiasi kwamba imekuwa ngumu kupata hati inayoshikilia mzee Kilomoni

Hali ya ugomvi wa Mkwabi na MO ulionekana wazi mara baada ya MO kuanza kuandika mfululizo wa ujumbe mbalimbali zenye “mafumbo” katika kurasa zake za kijamii na kuzidisha mijadala miongozi mwa wanachama, mashabiki wa Simba na wadau mbalimbali wa soka hapa nchini.

“Kwenye uongozi, na kwenye maisha, huwa nakaribisha kukosolewa. Lakini siwezi na sikubali kufanya kazi na mtu anayejuhumu malengo, mipango na maslahi mapana ya taasisi, mtu anayetoboa mtumbwi tunaosafiri nao,” MO aliandika ujumbe huo katika ukurasa wake huku akiweka picha inayomwonyesha Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe (kushoto) na kulia ni Mwenyekiti wa Simba, Swedi Mkwabi.

Kufuatia kutokuwa na maelewano baina ya hawo wawili, Swedi aliamua kujiweka pembeni kupisha mambo mengine tani ya klabu yaendelee.

Aidha, utaratibu wa kumpata Mwenyekiti mpya tutawatangazia hapo baadae.” imesema taarifa hiyo ya Simba.

 

 

Habari kubwa katika Magazeti ya Tanzania leo Septemba 15, 2019
Davido amvisha pete Chioma, harusi yaja