Uongozi wa Klabu ya Simba SC umeendelea kusisitiza kuwa Kiungo Mshambuliaji kutoka nchini Ghana Bernard Morrison, bado ni mchezaji halali wa klabu hiyo, kwa mujibu wa makataba uliopo baina ya pande hizo mbili.

Morrison anadaiwa kumalizana na Young Africans kwa kusaini mkataba wa miaka miwili, huku ikielezwa huenda akatambulishwa na Mabingwa hao Agosti 15 mwaka huu.

Mwenyekiti wa Simba SC Murtaza Mangungu amesema wanaendelea kumtambua kiungo huyo kama mchezaji halali wa klabu yao, na wanaheshimu mkataba uliopo kati yao na Morrison.

Amesema Mkataba wa Morrison utamalizika August 14, na Simba SC inaendelea kumlipa stahili zake kama kawaida ambazo ziliainishwa ndani ya Mkataba.

“Tunamtambua Morrison kama mchezaji wetu halali, bado ana mkataba wa Simba SC hadi Agosti 14, hatujawahi kusema popote kuwa mchezaji huyo sio halali kwetu, ndio maana tunasisitiza bado tunaendelea kumtambua, na stahiki zake analipwa kama wachezaji wengine ambao wana mikataba kwenye klabu yetu.”

Katika hatua nyingine Mangungu amesema, Simba SC inatambua Morrison aliondoka klabuni hapo kwa ruhusa maalum ya kwenda nyumbani kwao Ghana kwa ajili ya kutatua matatizo ya kifamilia.

Amesema wanayoyasikia anadai hakuwa na matatizo wanashangaa, lakini kabla ya kupewa ruhusa ya kuondoka na kurejea kwao Ghana, alidai ana matatizo binafsi na aliruhusiwa kwenda kuyatatua.

“Kuhusu yeye kusema hana matatizo ya Kifamilia nakataa hilo kwa kuwa ni Ukweli alipewa nafasi kwenda kupumzika kumalizana na mambo ya kifamilia na ipo kwenye maandishi kabisa.” Murtaza Mangungu

Mangungu: Ninamuheshimu sana Ismail Aden Rage
Habari kuu kwenye magazeti ya leo July 1, 2022