Kiongozi wa Azimio la Umoja nchini Kenya, Raila Odinga ametaka kufanyika kwa mageuzi katika Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka – IEBC, akisema utaleta uwazi wakati wa chaguzi.
Akihutuba wafuasi wake walijitokeza kwenye maandamano hii leo Julai 7, 2023 jijini Nairobi, Odinga amesema mabadiliko ya tume yataleta matokeo iwapo aliyekuwa mwenyekiti wa IEBC, Wafula Chebukati atakamatwa na kufungwa jela.
Amesema, “Chebukati alicheza na Wakenya kwa kuwanyima haki yao Kikataba kupata kiongozi waliyedhania angeingia Ikulu, tunataka Wafula Chebukati aingie ndani (jela).”
Katika uchaguzi mkuu wa Agosti 9, 2023 Raila Odinga aliwania urais kupitia mrengo wa Azimio, akimkabili Rais wa sasa William Ruto aliyemshinda na alifungua kesi kutaka matokeo ya urais yafutwe hata hivyo Mahakama ya Juu zaidi nchini humo ilimpa ushindi Ruto.
Maandamano ya Azimio yamefanyika ikiwa ni siku ya Saba Saba, inayofanyika Julai 7 kila mwaka ya ikiwa ni kumbukumbu ya oparesheni kutetea uhuru wa demokrasia Kenya na utawala wa vyama vingi iliyofanyika Julai 7, 1991.