Baada ya subira na vutankuvute ya muda mrefu, hatimaye Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC), Jecha Salim Jecha ametangaza rasmi tarehe ya marudio ya uchaguzi wa Zanzibar aliotangaza kuufuta Oktoba 28 mwaka jana.

Katika tangazo hilo, Jecha ameeleza kuwa kikao cha Tume hiyo kilichofanyika Januari 21 mwaka huu, kimeamua kuwa uchaguzi huo mkuu utarudiwa Jumapili ya Machi 20 mwaka huu.

Amesema kuwa uchaguzi huo utahusisha Rais, wajumbe wa Baraza la Wawakilishi na Madiwani na kwamba hakutakuwa na uteuzi wa wagombewa wala mikutano ya kampeni.

ZEC 1ZEC 2

'Zigo Remix' ya AY na Diamond yapigana vikumbo na nyimbo za Akon, Wiz Khalifa
Star wa Nigeria aendelea kusisitiza kuwa Wizkid amemuibia