Ili kuweza kuondokana na kutokomeza tatizo la wanafunzi kupata ujauzito wakiwa bado mashuleni, Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba amesema kuwa atazifuta taasisi zote zinazotetea haki za wanafunzi kupata mimba wakiwa mashuleni na mapenzi ya jinsia moja.

Mwigulu ameyasema hayo katika Harambee ya kuchangia ujenzi wa Parokia ya Kisasa mjini Dodoma ambapo alizungumzia kauli ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli kusema kuwa katika utawala wake hakuna mwanafunzi atakayeruhusiwa kuendelea na masoma akiwa mjamzito.

“Kwamimi ninayesimamia Idara ya utekelezaji wa maagizo nizionye taasisi zilizokuwa zikifanyia kazi Kampeni hizi, zitafute kazi nyingine, kama walidhani maelekezo ya Rais ni ajenda ya kuzua mijadala, nitazifutia usajii kama wakiendelea kutetea,”amesema Mwigulu

Hata hivyo, ameongeza kuwa kwa imani na maandiko aliyoyapitia yanazuia mimba za nje ya ndoa na pia mimba za utotoni hivyoanawashangaa wale wote wanaopigania na kuendesha kampeni kama hizo.

Saida Karoli: Nimekaa jela miaka 15
Kamati ya TFF yatoa uamuzi wa mwisho uchaguzi Lipuli FC