Mbunge wa Iramba Magharibi, Dkt Mwigulu Nchemba amesema upo umuhimuwa kufanya utafi ti kujua ni kwanini pamoja na ushindi mkubwa iliopata CCM katika Uchaguzi Mkuu mwaka huu, watu waliopiga kura walikuwa wachache jimboni humo.
Mwigulu amesema hayo wakati akizungumza kwenye kikao cha Halmashauri ya CCM wilayani humo kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya mji wa Kiomboi.
Amesema idadi ya wapigakura asilimia 30.34 isiyofika nusu ya watu 141,521waliojiandikisha jimboni humo ilikuwa ni ndogo ikilinganishwa na wapiga kura waliojiandikisha kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga kura.
“Tumeshinda kwa kiwango kikubwa kwenye nafasi ya urais, mbunge na madiwani lakinikuna kiporo cha kukifanyia kazi kwani idadi ya watu waliojitokeza kupigakura ni ndogo kuliko ya waliojiandikisha,” amesema.
“Hili ni jambo la kufanyiwa kazi kwa haraka kwani katika tathmini za kiushindani linapaswakupatiwa majibu ikiwamo kubaini chanzo cha tatizo hilo,”amesisitiza
Katika hatua nyingine,Mwigulu amewasihi Watanzania kuunga mkono juhudi zamaendeleo zinazofanywa na Rais John Magufuli kwani rekodi ya utendaji kazi aliyofanyakwa wananchi wa Tanzania katika huduma mbalimbali za kijamii haina kifani na itatumikakama somo duniani kote.