Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage amesema kuwa sukari ipo ya kutosha na kilichojitokeza zilikuwa Propaganda za watu waliokuwa na ajenda yao binafsi.

Ameyasema hayo Bungeni Jijini Dodoma alipokuwa akihitimisha hoja ya bajeti ya Wizara yake ya mwaka 2018/19, ambapo amesema kuwa tayari amesha liagiza Shirika la Viwango Tanzania (TBS) na Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) kutoa sukari yote iliyopo Bandarini.

Amesema kuwa hapendi kuona waumini wa Kiislam wakipata shida wakati wa mfungo wa mwezi wa Ramadhan unaotarajiwa kuanza hivi karibuni.

“Viwanda vya Sukari vyote nchini bado kama wiki tatu tu vinaanza kuzalisha, suala hili lilikuwa ni Propaganda tu, na mimi ni ‘Propagandist’ niliyesomea China,”amesema Mwijage

Hata hivyo, kuhusu mazingira ya uwekezaji, amesema kuwa amekuwa akipigania kuyafanya yawe rafiki na kuwaomba wabunge kutoa ushirikiano pale wanapoona kuna changamoto.

 

Wasiokuwa na vyeti vya kuzaliwa, ndoa kuzisikia hewani
Serikali yataifisha Migodi ya Madini nchini