Serikali imepiga marufuku kuwakata fedha wanazopewa wanufaika wa mfuko wa maendeleo ya jamii nchini Tanzania (Tasaf) kuchangia miradi ya maendeleo.

Waziri wa nchi ofisi ya Rais (Utumishi na utawala bora) George Mkuchika amesema hayo wakati wa hafla ya uzinduzi wa kipindi cha pili cha awamu ya tatu ya Tasaf Jijini Dar es Salaam.

Amesema kuwa haiwezekani wanufaika hao wakatwe fedha za maendeleo ikiwa ni pamoja na ujenzi wa shule za sekondari wakati wenye uwezo wa kutoa michango hiyo hawajafanya hivyo

” Katika baadhi ya mamlaka za serikali za mitaa wakiwa na hela ya michango ya sekondari, hela raisi kuipata ni ya Tasaf wanaenda kuikata niliagiza zile halmashauri warudishe hela zao” amesema Mkuchika

”Michango ya maendeleo wanapaswa kuchangia watu wenye uwezo, hawezi mtu apewe 20,000 akapambane na uaskini unakata mchango wa sekondari wakati aliye na uwezo hakatwi hata shilingi moja” amesema waziri Mkuchika

Ameongeza kuwa wanufika wanasimamiwa kwa hiari yao kujiunga na vyama vya ushirika bima za afya na maeneo mengine.

 

Castle Lite Unlock kufungua milango ya tiketi Februari 20 kwa punguzo, msanii mkubwa wa hip hop Afrika kutumbuiza
Lukuvi atimiza agizo la Rais Magufuli akabidhi ekari 715 Kigamboni