Mwanamke, Mercy Mkandara anayedaiwa kuuawa na mumewe wa ndoa, Erick Samson, mwiliwake unatarajiwa kuagwa leo katika hospitali ya Tumbi, Kibaha mkoani Pwani.
Baada ya kuagwa mwili huo utasafirishwa kwaajili ya maziko nyumbani kwao Bukoba mkoani Kagera ambapo utapitia kwanza Mwanza kwenye makazi ya wazazi wake.
Taarifa ya kuagwa kwa marehemu Mercy imetolewa na mmoja wa nduguzake ikiwa ni uamuzi wa kikao kilichofanyika kati ya ndugu wa wanando hao na kukubaliana azikwe upande wa mwanamke.
Kamanda wa polisi Kinondoni, Edward Bukombe amesema tayari mtuhumiwa ambaye ni mume wa marehemu amehojiwa na utaratibu unafanyika ili kumpeleka Mahakamani.
Mercy alifariki dunia usiku wa kuamkia Juni 16, 2020, huku Mumewe akieleza kuwa kifo chake kimetokana na shoti ya umeme licha ya majiriani zake kutilia shaka sababu hiyo kwani alikutwa na majeraha makubwa kichwani.