Jana August 30, 2017 Mkurugenzi Mtendaji  wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete  (JKIC), Profesa Mohamed Janab ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa moyo wa mfanyabiashara Yusuf Manji umewekwa vyuma ili kumsaidia kupumua.

Profesa Janab amesema hayo mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Cyprian Mkeha wakati akitoa ushahidi katika kesi ya madawa ya kulevya inayomkabili mfanyabiashara huyo.

Ambapo ameeleza kuwa Februari 2017, Manji alifikikishwa kwenye Taasisi na kufanyiwa vipimo vya moyo na jopo la madaktari na kubaini kuwa moyo wake umewekewa vyuma lakini upo katika hali nzuri.

Pia Profesa Janab ameulizwa kuhusu mgonjwa aliyewekewa vyuma katika moyo kama anaweza kutumia dawa za kulevya.

Ambapo amejibu kwa kusema, kutokana na hali hiyo mgonjwa haruhusiwi kufanya baadhi ya mambo ikiwemo kuvuta sigara, kutumia heroin.

”Hivyo kama akitumia athari zake ni kwamba mirija ya moyo itaziba, kisha atatakiwa afanyiwe upasuaji mkubwa zaidi”.

Profesa Janab ameieleza mahakama kutokana na majibu yaliyotolewa na mkemia mkuu kuwa mkojo wa Manji uligungulika kuwa na chembe za Heroin, lakini cha kushangaza ni kwamba athari za dawa hizo bado hazijaonekana kwenye moyo wa mshtakiwa ambapo ingepelekea kufanyiwa upasuaji mkubwa zaidi kutokana na mirija hiyo kuziba na kushindwa kusafirisha damu kama ilivyo kawaida.

Aidha kutokana na ushahidi uliotolewa Mfawidhi, Cyprian Mkeha amesema ameridhika na utetezi huo na mshtakiwa anayo haki ya kujitetea zaidi na kuleta mashahidi.

Manjia alifikishwa mahakamani hapo kwa mara ya kwanza Februari 26, mwaka huu akidaiwa kuwa ametumia dawa za kulevya aina ya Heroin.

Kesi yake inaendelea leo kwa ajili ya kuendelea na ushahidi.

 

 

Mpinzani wa Kagame apotea, polisi wanawa mikono
Haji Manara afichua siri ya benchi la ufundi