Mwili wa aliyekuwa mbunge wa viti maalum wa Manyara kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Martha Umbulla, utaagwa leo Januari 23, 2021, katika viwanja vya Bunge jijini Dodoma.

Martha alifariki dunia usiku wa kuamkia Januari 21, 2021, nchini India katika hospitali ya HCG Mumbai, alipokwenda kwa ajili ya kupatiwa matibabu.

Taarifa ya kifo chake ilitolewa na Spika wa Bunge la 12, Job Ndugai, na kueleza kuwa ofisi ya Bunge kwa kushirikiana na familia itaratibu mipango yote ya mazishi.

Kwa upande wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli, ametuma salamu za rambirambi na kueleza jinsi gani alivyokuwa akimfahamu Martha, na kuongeza kuwa alikuwa ni mpole, mchapakazi na mpenda maendeleo.

Faida ya boga kwa wanawake waliopo katika umri wa kuzaa
Zanzibar yaupa kipaumbele uchumi wa bluu