Familia ya Mwanamuziki Nipsey Hussle imethibitisha kuaga rasmi mwili wa msanii huyo Aprii 11, 2019 katika ukumbi wa Staples Center Mjini Los Angeles.

Aidha, taarifa zimeripotiwa kuwa tiketi zimeanza kuuzwa matandaoni kwa ajili ya kuingia katika ukumbi huo wenye uwezo wa kubeba jumla ya watu 21,000  ambapo wenye tiketi pekee ndiyo watapata nafasi ya kuingia.

Ukumbi huo ndiyo uliotumuka kuaga mwili wa Mfalme Pop Marehemu Micheal Jackson mwaka 2009.

Naye msanii wa rap, Kodak Black ameibua hasira za mashabiki na baadhi ya wasanii  baada ya kutoa kauli akiwa ‘live’ kwenye instagram yake ambayo haikuwafurahisha wengi katika kipindi hiki cha kuomboleza kifo cha mwanaharakati Nipsey Hussle.

”Lauren London ni mjane na kwa kuwa anampenda basi atamrithi kwa muda wa mwaka mmoja akimfariji na kumpooza katika kipindi hiki kigumu cha kumlilia mumewe” alisema Kodak  black

Hata hivyo kituo cha radio cha power 106 cha mjini Los Angeles kimetangaza kutopiga muziki wa Kodak black kufuatia kauli aliyoitoa, The game na T.I wametoa ya kwao ya moyoni huku baadhi ya wasanii nchini Marekani wakichukizwa na kauli hiyo.

Nipsey Hussle alifariki Marchi 31,2019 baada ya kupigwa risasi nje ya duka lake ‘The MarathonClothes’ Mjini Los Angeles.

Mashabiki waizila show ya kwanza ya R Kelly
ACT - Wazalendo: Maandamano yapo pale pale, Kamanda afuate katiba

Comments

comments