Meneja wa Habari na Mawasilino wa Simba SC Ahmed Ally amesema kesho Jumatano (Julai 13), klabu hiyo itamtambulisha mchezaji wapili wa Kimataifa aliyesajiliwa kwa ajili ya msimu mpya wa 2022/23.
Simba SC tayari imeshawatambulisha wachezaji wa kigeni Victor Akpan (Nigeria) na Moses Phiri (Zambia), huku wachezajai wazani ni Nassoro Kapama na Habib Kyombo.
Ahmed Ally amethibitisha taarifa za kuthibitishwa kwa mchezaji mwingine wa kigeni kesho Jumatano (Julai 13) alipozungumza katika Mkutano na Waandishi wa Habari leo Jumanne (Julai 12), Hoteli ya Serena jijini Dar es salaam.
Ahmed amesema utambulisho wa mchezaji huyo sio tu Afrika itatikisika, bali Dunia nzima itasimama kutokana na ukubwa wa jina lake na takwimu za soka alizozibeba.
“Ni mchezaji ambaye Quality yake haijawahi kucheza hapa Tanzania, ni kwa mara ya kwanza atakua anatua hapa Dar es salaam, kwa hiyo niwahakikishie Wanasimba kuwa kesho kuna balaa kubwa, na sio wachezaji ambao wamefili sehemu nyingine, huyu ni mchezaji ambaye ameproove takwimu zake, ubora wake, kesho tunakwenda kumuweka hadharani.”
“Kwa hiyo ukifika muda wa Saa Saba kamili mchana, niwaombe tu Waandishi wa Habari na Wanasimba wajiandea kufuatilia nini kinakwenda kutangazwa katika kurasa zetu za Mitandao ya Kijamii na Simba APP.” amesema Ahmed Ally
Simba SC inahusishwa na mpango wa kuwasajili Cecar Lobi Manzoki (Jamhuri ya Afrika ya Kati), Nelson Okwa (Nigeria) na Augustine Okra (Ghana).