Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Alhaji Ali Hassan Mwinyi wameshauriwa vijana nchini kujitolea na kuwatunza wazee katika maeneo yao ili kupata ushauri na busara za wazee hao kwa maendeleo yao na taifa.

Mwinyi amesema hayo alipokuwa akizungumza na wazee katika kilele cha maadhimisho ya Siku ya Wazee Duniani yanayofanyika kila Oktoba Mosi ya kila mwaka.

Amesema kuwa jukumu la kuwatunza na kuwalea wazee sio la Serikali pekee bali jamii  pia ina nafasi yake katika kuwatunza wazee hasa Vijana.

Ameongeza kuwa Serikali imejitaidi sana kuweka mazingira mazuri kwa wazee kwa kuwapatia huduma za Afya na kuwatunza wazee wote ambao hawana ndugu wa kuwatunza katika makambi mbalimbali ya wazee nchini.

“Niwaombe vijana mtutunze sisi wazee kwani na sisi tulikuwa vijana kama ninyi na mkiweka utamaduni huu utawasaidia na ninyi mkiwa wazee hapo baadae” amesema Mwinyi.

Naye Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amemhakikishia Rais Mstaafu, Mwinyi kuwa Serikali itaendelea kuwatunza wazee nchini na kuhakikisha wanapata hudumu zote muhimu.

“Nikuhakikishie Mwinyi kuwa tutaendelea kuwatunza wazee kwa kuwapatia huduma muhimu hasa huduma za Afya” amesema Ummy.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Mtandao wa Wazee nchini, Mzee Sebastian Bulegi amemuomba Mwinyi kufikisha shukurani  zao kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa moyo wake wa kuwajali wazee nchini.

“Mwinyi naomba utufikishie shukurani zetu kwa Rais Magufuli kwa kutujali wazee hasa kwa kutatua changamoto zetu zinazotukabili” alisema Mzee Sebastian.

Kila Mwaka, Oktoba Mosi siku ya Wazee Duniani huadhimishwa kufuatia Azimio la Umoja wa Mataifa linalozitaka nchi wanachama kutenga siku maalumu ya kutafakari mchango wa Wazee katika maendeleo ya jamii na kuwaenzi ili wawe  na maisha bora na yenye matumaini na Kauli mbiu ya Maadhimisho ya Mwaka huu ni “ Kuelekea uchumi wa Viwanda:Tuthamini Mchango, Uzoefu na Ushiriki wa Wazee kwa maendeleo ya Taifa”.


Video: HATARI!! “Tulivunja shule baada ya kukosa hela, wazazi wangu walinifanyia kitu cha ajabu sana”.

Dkt. Kikwete aibukia shule aliyosoma, aliliwa matatizo
Viongozi wa dini watakiwa kuwapiga vita wanaotaka kuvuruga amani nchini