RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi ametangaza rasmi Baraza jipya la Mawaziri Zanzibar, ambapo jumla ya Wizara 15 zimepata Mawaziri na kuacha nafasi katika Wizara mbili.

Rais Mwinyi amesema ameacha wazi nafasi hizo ambazo ni za Waziri wa Afya na Waziri wa Biashara kwa ajili ya ACT-Wazalendo kama chama hicho kitakuwa tayari.

Aidha, Dkt Mwinyi amesema aliwaandikia barua chama cha ACT-Wazalendo kupeleka jina la Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar, kama katiba inavyotaka lakini hawajapeleka.

Rais Mwinyi hajateua naibu waziri yeyote katika baraza hilo, na atateua endapo ataona kuna wizara inahitaji naibu.

Uwanja wa Jamhuri ruhsa kutumika VPL
Hili hapa Baraza jipya la Mawaziri Zanzibar