Kiungo Mchezaji, Mwinyi Kazimoto amejiunga tena na klabu ya Simba akitokea klabu ya Al Markhiya ya Qatar. Mwinyi amerejea Simba baada ya kujiunga na Al Markhiya ambayo alitimkia akitokea Msimbazi. Ameichezea timu hiyo ya daraja la pilim misimu miwili lakiini timu hiyo ikashindwa kupanda daraja.

Kutokana na hali hiyo, uongozi wa Al Markhiya uliamua kubadili asilimia kubwa ya wachezaji ilionao ili kuleta mabadiliko yatakayoiwezesha kupanda daraja. Fagio hilo la mabadiliko lilimkumba Kazimoto.

Hata hivyo, Kazimoto alikuwa na bahati kwa kuwa wakati mabadiliko yanafanyika, tayari alikuwa amepata ofa ya kujiunga na Petrojet inayoshiriki Ligi Kuu Misri.

Licha ya juhudi za Petrojet kutaka Kazimoto ajiunge na timu yao, yeye alisisitiza kuwa anataka kurejea nyumbani  nia ambayo hatimaye ameitiza na kutua tena kwa wekundu wa Msimbazi.

“Ni kweli tumefanya juhudi kumshawishi kwamba Petrojet ingekuwa changamoto nzuri kwake. Lakini alikataa katakata na akasisitiza anataka kurejea nyumbani, hatukuwa na ujanja.
“Kibaya kwa wachezaji wa Tanzania, wengi wanataka kubaki Tanzania, ni waoga wa changamoto,” kilieleza chanzo cha uhakika kutoka ndani ya al Markhiya huko Qatar.

CCM Yajipanga Kuwajibu Chadema Na Lowassa Leo
Mbowe Na Lowassa ‘Waliudanganya’ Umma Kuivuruga CCM