Mgombea urais kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar, Dkt. Hussein Mwinyi ameeleza zababu za kuwania nafasi hiyo kuwa ni kuwatumikia wazanzibari.

Ameyasema hayo leo Agosti 26, 2020 wakati akichukua fomu ya uteuzi kutoka Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC).

Aidha Dkt Mwinyi ameongea na wanachi ambapo ameahidi kuleta mabadiliko katika sekta ya viwanda na utalii ambazo zitachangia vijana kupata ajira.

“Nimeamua kugombea nafasi hii kwa dhamira moja tu, nayo ni kuwatumikia Wazanzibar, kwahiyo kuweni na matarajio na Inshaallah mwenyezi Mungu akitujalia kwa kushirikiana tutayatimiza“, amesema Dkt Mwinyi.

Sisi sote tuhakikishae tunahubiri amani na kila mmoja ahakikishe anailinda amani bila ya amani hakuna maendeleo ,bila ya amani hata ibada hatutazifanya tuhakikishe tunailinda amani tuliyonayo amesema Dkt. Mwinyi.

Aidha Dkt Mwinyi amewaasa wazanzibar, kuhakikisha wanailinda amani walionayao kwani hakuna maendeleo yatakayokuja kisiwani hapo kama hakuna amani.

Moto wateketeza mabweni shule ya African Muslim
Zahera: Wanaombeza Yondani hawajui mpira