Mashabiki wa Chelsea wanaamini winga Mykhailo Mudryk atawaongoza katika ushindi dhidi ya Arsenal kwenye mechi ya Ligi Kuu England mwishoni mwa juma hili.
Mudryk mwenye umri wa miaka 22, alifunga bao kwa mara ya kwanza kabla ya mapumziko mechi ya kimataifa dhidi ya Fulham na Jumanne usiku aliibuka kinara kwa taifa lake.
Staa huyo wa kimataifa wa Ukraine alifunga bao kwa taifa lake dhidi ya Malta kwenye mechi ya kufuzu Euro 2024 akiwapa matumaini mashabiki wa Chelsea.
Winga huyo aliyesajiliwa kwa Pauni 88 milioni alionyesha kiwango kizuri dhidi ya Malta katika ushindi wa mabao 4-1.
Mudryk alifunga bao la shuti kali nje kidogo ya eneo la hatari baada ya kukokota mpira na kumpita beki wa Malta.
Mashabiki wa Chelsea walifurahishwa na kiwango chake na kumsifia kupitia mitandao ya kijami.
Shabiki mmoja aliandika: “Hili bao ni la dunia nyingine kabisa.”
shabiki mwingine akasema “Mashabiki wa Arsenal mjiangalie”
Shabiki wa tatu akakomenti: “Kijana anaweza kuwa moja ya mawinga hatari sana duniani”
Mwingine alihamaki akiandika: “Hivi kweli huyu ni Mudryk? jamani niamsheni.”