Klabu ya Chelsea inaamini winga wake Mykhailo Mudryk ataanza kucheza kwa kiwango chake hivi karibuni baada ya kusuasua tangu alipojiunga na wababe hao wa Stamford Bridge katika dirisha dogo la usajili msimu uliopita.

Winga huyo aliigharimu Chelsea Pauni 88 milioni lakini hakuweza kutoboa katika kikosi cha kwanza na ameendelea kusuasua msimu huu, hata hivyo, bado ana mkataba wa miaka minne na ana nafasi ya kuonyesha ubora wake.

Mwenyekiti wa Chelsea, Todd Boehly alitoa Pauni 62 milioni kwanza kwa ajili ya winga huyo na zilizobaki zitamaliziwa baadae ikiwamo bonasi endapo watabeba mataji.

Sasa inaelezwa winga huyo hajafikia asilimia ambayo Chelsea ingelipa awamu nyingine ya pesa iliyobaki kwa sababu bado hajamshawishi kocha wake Mauricio Pochettino aliyechukua nafasi ya Graham Potter.

Mudryk alicheza mechi yake kwanza Januari mwaka huu na kudumu kwa dakika 45 ambayo Chelsea iliambulia sare ya 0-0 dhidi ya Fulham katika mchezo huo wa Ligi Kuu England na hadi sasa baada ya mechi 20 hajafunga bao hata moja, huku msimu huu amecheza dakika 67 katika mechi nne akitokea benchini. Inaelezwa kwa sasa Mudryk anahitaji uzoefu na kupewa muda wa kutosha wa kucheza.

Ahmed Ally: Tunataka heshima yetu idumu
Kocha Middendorp aisoma Future FC