Wakati sakata la kiungo wa Simba SC Mzamiru Yassin la kuhusishwa kuihama timu hiyo na kutua Yanga, mchezaji huyo amesababisha gumzo lingine kuhusu usajili wake.

Taarifa hizo zimekuja wakati huu ambapo kuna dirisha dogo la usajili lililofunguliwa tangu Novemba 15, mwaka huu.

Mzamiru amezua gumzo hilo kupitia ukurasa wake wa Instagram, ambapo ameandika ujumbe huu:

“Wakati unapofanya maamuzi kwa wakati maalumu huna budi kumshukuru mwenyezi Mungu kwani bila yeye wewe si kitu, waachie walimwengu waendelee kuongea midomo mali yao.”

Mara baada ya ujumbe huo ikaonekana kama maamuzi anayoyazungumzia ni kuelekea Yanga, lakini alipoulizwa Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara alisema hajui chochote kuhusu suala hilo kwa kuwa Mzamiru bado ni mchezaji wa Simba SC.

Makala: Saa chache za kuanika ya Kubenea, Mnyika, Sakaya ‘kutimkia CCM’
Elias Maguli azikacha klabu kongwe, atimkia bondeni