Hatimaye mzee mkongwe katika baraza la wanayanga Yahya Akilimali amesimamishwa rasmi uanachama licha ya kujitetea na kujisafisha.

Katika mkutano wa dharura uliofanyika Jangwani leo asubuhi mzee Akilimali alikiri kauli zake na kuwasilisha utetezi.

“Katika watu tunaompenda Manji, mimi namba moja lakini ikumbukwe Mwana umleavyo ndivyo akuavyo, Manji alikuwa anatuita akitaka kufanya jambo. Ila siku hizi hatuiti hatuambii lolote anafanya tu, nimemwambia Manji, mimi ndio nimempa ukuu wa Yanga. Sisi tunampenda kweli Yusuf na nimemtaka radhi jana”.

“Labda niseme hivi Kama kukurupuka ni Tusi kama nilivyomwambia Yusuf, basi naomba radhi kwake Manji na wanayanga wote”.

Licha ya kuwasilisha utetezi huo kikao Cha viongozi wa Matawi ya klabu ya Yanga imemsimamisha Katibu wa baraza la Wazee, Yahya Akilimali kwa kile kinachoitwa kumkashifu Mwenyekiti wa klabu hiyo kongwe nchini Yusuph Mehboob Manji.

 

Picha: Mazishi ya Rais wa Awamu ya Pili wa Zanzibar, Alhaj Abood Jumbe
Amissi Tambwe Arejesha Majibu Kwa Wanaotaka Ushindani