Katibu wa Baraza la Wazee wa Yanga, Mzee Ibrahim Akilimali amemtaka Msemaji Mkuu wa Klabu ya Simba, Haji Manara kupunguza maneno baada ya kushindwa kutamba mbele ya Ndanda FC kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara kwa kutoka nayo suluhu ya kutokufungana.

Mzee Akilimali ameibuka na kumpa pole Manara akisema kuwa ni mdogo wake na hawezi sana kumtania japo amemuomba kupunguza zaidi maneno kuliko vitendo.

“Unajua huyu mdogo wangu nadhani bado hajaitambua ligi vizuri, namshauri tu vizuri kwa maana siwezi kumtania ni vema akaelewa kuwa mchezo una matokeo matatu. Namuomba apunguze zaidi tambo kwa timu yake na atambue kuwa si kila mechi unaweza kushinda” amesema.

Msemaji wa Klabu ya Simba, Haji Manara

Amemtaka Manara kupunguza zaidi tambo za kujigamba na badala yake amemuelewesha kuwa kwenye mchezo huwa kuna matokeo matatu.

Akilimali ameongeza kuwa Manara amekuwa akiwatania zaidi Yanga huku akiipa sifa kubwa Simba na kusahau kama mpira huwa na matokeo ya aina yake.

Mzee huyo anaamini suluhu waliyoipata Simba dhidi ya Ndanda itakuwa imewapa funzo.

Habari kubwa katika magazeti ya Tanzania leo Septemba 17, 2018
NEC yaelezea kuhusu Mawakala waliokatatiliwa