Mzee aliyebuni nembo ya taifa, Francis Kanyasu maarufu kwa jina la Ngosha amefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika hospitali ya taifa ya muhimbili alikokuwa amelazwa kwaajili ya kupatiwa matibabu.

Taarifa iliyotolewa kwa umma na Hospitali hiyo imesema kuwa marehemu alifikishwa hospitalini hapo akitokea hospitali ya Amana siku ya Alhamis Mei 25 mwaka huu saa tano asubuhi.

Aidha, taarifa hiyo imesema kuwa tangu afikishwe katika hospitali hiyo, kumekuwepo na jitihada kubwa ambazo zilikuwa zikifanywa ili kuweza kuokoa maisha yake kwa kumpatia tiba na huduma zote mpaka jana usiku alipofariki.

Utafiti: Bodaboda, baiskeli hatari kwa nguvu za kiume
Mamlaka ya hali ya hewa yatoa tahadhari kwa wakazi wa ukanda wa pwani