Mkongwe wa Filamu za Kibongo nchini, aliyejipatia umaarufu kwa kuigiza vichekesho, Amri Athumani ‘Mzee Majuto’, aliyeanza kuagiza mwaka 1958 akiwa na miaka 10, ambaye mwaka jana aliwahi kutangaza kuacha uigizaji na kumrudia Mungu, amesema ataendelea kuigiza hadi anakufa kwa sababu uigizaji upo kwenye damu na hii inadhihirishwa wazi kwani ni miaka 58 sasa ya uigizaji wake na fani hii ameianza akiwa darasa la pili.

Amezungumza hayo Dar es salaam Jana, Mzee Majuto amesema hawezi kukubali kuona fani inachezewa na watoto, hivyo ataendelea kuigiza hadi siku atakayokufa kwa sababu uwezo wake ni wa hali ya juu kwenye kuandika na kuigiza.

”Kuigiza kwangu ni kama maradhi vile, hivyo sidhani kama naweza kuacha, siwezi kukaa pembeni sanaa ikawa inachezewa na watoto sitaki kabisa,  nitaendelea kuigiza hadi nakufa,” amesema Majuto.

Mzee Majuto aliongeza anaendelea kuigiza lengo ili kuhakikisha anapata chipukizi ambaye anaweza kufanya kile alichokuwa anakifanya yeye hapo baadae.

Amesema bado hajapata mtu wa kurithi mambo yake katika tasnia hiyo, hivyo hawezi akakurupuka kuachana na kazi hiyo bila ya faida ambayo kwa upande wake ni kupata mrithi.

 

Asili ya mikono inayojali ni moyo unaojali
Lissu aibebesha zigo CCM kufungwa kwa Lijualikali