Muigizaji maarufu wa Kenya, Benson Wanjau maarufu kama Mzee Ojwang anatarajiwa kuzikwa leo (Julai 29) katika eneo la Lang’ata nchini Kenya na maandalizi makubwa ya mazishi yamefanyika.

Ili kuhakikisha wanampa heshima ya mwisho kwa namna inayostahili, watu maarufu wa Kenya walikusanyika katika uwanja wa Nyayo kufanya mazoezi ya jinsi ya kushiriki vizuri katika kutoa heshima ya mwisho kwa marehemu Mzee Ojwang.

Lengo kubwa la mazoezi hayo ni kuwafariji wageni mbalimbali watakaohudhuria mazishi na watakaokuwa wakiyafuatilia kwenye runinga wakiwa nyumbani.

Mchekeshaji huyo mkongwe wa kipindi cha Vitimbi alifariki mwezi uliopita katika hospitali ya taifa ya Kenyatta alipokuwa akipatiwa matibabu kutokana na matatizo ya maumivu ya kifua.

Ingawa Mzee Ojwang alikuwa maarufu sana, hali yake ya kiuchumi haiendana na umaarufu wake na kuripitiwa mara kwa mara kuhangaika na kipato kidogo. Baadhi ya waigizaji wa kipindi cha Vitimbi kilichokuwa kinarushwa kupitia kituo cha runinga cha KBC walilalamikia serikali kuwa imewatenga.

Adebayor Anukia Aston Villa Ya Tim Sherwood
Wenger Arudisha Majibu Kwa Mourinho