Medadi Chitezi mwenye umri wa miaka 60, mkaazi wa Kijiji cha Ulumi, Wilaya ya Kalambo, Mkoa wa Rukwa amehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela, baada ya kukutwa na hatia ya kumbaka msichana mwenye umri wa miaka 10.

Akisoma hukumu dhidi yake, Hakimu Nixon Temu alisema kuwa baada ya kusikiliza pande zote mbili, Mahakama imebaini kuwa Chitezi alifanya kosa hilo Agosti 12, 2020 majira ya usiku, kinyume cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu, Sura ya 130.

Alisema kuwa ingawa Chitezi alikana mashtaka dhidi yake, baada ya kukamilisha mchakato wa kusikiliza shauri hilo, Mahakama ilijiridhisha pasipo na shaka kuwa alitenda kosa hilo.

“Kosa lililofanywa na Chitezi ni la kinyama na kinyume cha ubinadamu. Ingawa alikana mashtaka dhidi yake, kwakuwa amepatikana na hatia pasipo na shaka yoyote, anastahili adhabu kali dhidi yake ili iwe fundiso sio kwake tu bali pia kwa watu wenye tabia kama hizi,” amesema Hakimu Temu.

Baada ya kupewa nafasi ya kujitetea, Chitezi aliiomba Mahakama imsamehe kwakuwa alifanya kosa hilo akiwa amelewa.

Utetezi wake hakuzaa matunda, na adhabu ya kifungo cha miaka 30 jela ikabaki dhidi yake.

NEC yawarejesha wagombea 24 wa udiwani kwenye uchaguzi
Habari kubwa kwenye magazeti leo, Septemba 13, 2020