Mchungaji Anthony Lusekelo maarufu kama Mzee wa Upako amewataka wanasiasa kutowafuata viongozi wa dini kwa lengo la kuwatumia katika harakati zao za kisiasa.
Akizungumza hivi karibuni katika majadiliano maalum kupitia Channel 10, mjadala uliowakutanisha viongozi wawili wa dini, Mzee wa Upako alisema kuwa kuwa ni hatari kuona dini inachanganywa na masuala ya kisiasa kwa kuwa jambo hilo linaweza kupelekea machafuko.
“Sisi viongozi wa dini tunapaswa kuwa watu wa mwisho kufuatwa pale ambapo mambo yanaharibika,” alisema. “Sasa kama tunafuatwa na wanasiasa kwa ajili ya kutumiwa kwenye siasa nani atasaidia kutuliza mambo yakiharibika?” alihoji na kuongeza kuwa viongozi wa dini pia wanapaswa kutowafuata wanasiasa hususan katika kipindi hiki cha uchaguzi.
Katika hatua nyingine, Mzee wa Upako alieleza kuwa hata vikundi maalum vya bodaboda na mama lishe ambavyo viliundwa kwa malengo mbalimbali havipaswi kutumika kwa umoja huo kwa masuala ya kisiasa kwa kuwa hiyo sio sababu iliyoviunda vikundi hivyo kisheria.
Mjadala huo uliokuwa na mada isemayo ‘Nasaha ya viongozi wa dini kuelekea Uchaguzi Mkuu’ na ulihudhuriwa na mchungaji huyo pamoja na Sheikh aliyewakilisha dini ya Kiislamu.

Lowassa: CCM Wamekumbuka Shuka Kumekucha
Mambo Kumi Unayomwambia Mwanao Kimakosa Karibu Kila Siku