Mfalme wa muziki wa taarab, Mzee Yusuf amezungumzia kile kinachoaminika kuwa beef kati ya Diamond na Ali Kiba kinachoitawala mitandao ya kijamii na kuunda timu za kupambana kwa maneno makali.

Diamond na Ali

Mzee Yusuf amesema kuwa yeye haamini kama wawili hao wana ugomvi wa aina yoyote kwa kuwa wawili hao wawajawahi kukutana na kukwaruzana au kupigana ngumi ili kudhirisha ugomvi wao. Alisema beef la kweli liko hasa muziki wa Taarab.

“Kwenye taarab kuna beef za kweli, watu wanazipiga kweli. Mimi naamini wanaume hawanuniani,” Mzee Yusuf aliuambia mtandao wa Bongo5.

Alisema kuwa ugomvi kati yao unachochewa na mashabiki huku akieleza pia kuwa ana mpango wa kuanzisha umoja wa wasanii wa muziki wa Taarab.

Kufuli la Rais Magufuli lawaliza wafanyabiashara Dodoma
Rais Magufuli amteua Hamphrey Polepole Kuwa Mkuu wa Wilaya Musoma