Mshambuliaji wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Young Africans aliyefunga bao lililowapeleka kwenye makundi la Ligi ya Mabingwa Afrika kwa mara ya kwanza baada ya miaka 25, Clement Mzize ametuma salamu nzito kwa kinara wa mabao wa sasa Ligi Kuu kutoka Simba SC Jean Baleke.

Mzize ambaye hakutaja moja kwa moja kuwa salamu hizo ni za Baleke, amesema kuwa anataka kukumbukwa kwa kufunga mabao mengi kwenye kila msimu na kazi hiyo anataka kuianza msimu huu 2023/24.

Mzize alikazia kuwa hataki kutajwa kuwa alitoa asisti nyingi ndani ya msimu mmoja, yeye anataka kukumbukwa kwa kuwa mchezaji ambaye alifunga mabao mengi kwenye msimu mmoja na kwa malengo makubwa aliyonayo atafikia kwenye hatua hiyo.

Hadi sasa Baleke ndiye kinara wa mabao akiwa amefunga mabao matano kwenye mechi tatu, huku Mzize akiwa anajitafuta kwenye ligi na jumla kwenye michuano yote amefunga mabao manne.

“Watu waliona kazi yangu ambayo nilifanya msimu uliopita. Niliaminiwa na nikafanya kazi, msimu huu nina malengo makubwa sana, sitaki kukumbukwa kwa kutoa asisti nyingi.

“Nataka kukumbukwa kwa kuwa mchezaji ambaye amefunga mabao mengi ndani ya msimu mmoja,” amesema Mzize.

Jafo aipongeza NEMC usimamizi sheria ya Mazingira
Askari Polisi waonywa matumizi ya Vilevi kazini