Rais wa Marekani, Joe Biden anatarajiwa kuzuru Israel hapo kesho Jumatano Oktoba 18, 2023 kuthibitisha kujitolea kwa Marekani kwa usalama wa Israel hatua inayokuwa wakati wito wa Mataifa mengi ukiongezeka kwa Israel ili iweze kufungua njia na kuruhusu misaada kuingia Gaza.

Ziara hiyo ya Rais Joe Biden nchini Israel, imetangazwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Antony Blinken ambaye amesema Biden pia atathibitisha uungaji mkono wa Marekani kwa Israel na kujitolea kwa mambo mbalimbali ya kiusalama kwa Israel.

Amesema, Israel ina haki na wajibu wa kuwalinda raia wake dhidi ya Hamas na makundi mengine ya kigaidi na kuzuia mashambulizi ya siku za usoni na kwamba amekubaliana na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu kuhusu mpango utakaowezesha misaada ya kibinadamu kuwafikia raia ndani ya Gaza.

Hata hivyo, Waziri wa Ulinzi wa Israel, Yoav Gallant ambaye alizungumza na Waandishi wa Habari baada ya kukutana na Blinken alisema, “hivi vitakuwa vita vya muda mrefu na gharama itakuwa kubwa. Lakini tutashinda kwa ajili ya Israeli na Wayahudi na kwa maadili ambayo nchi zote mbili (Israel na Marekani) zinaamini.”

Afya ni aisha yako, furahi fanya mazoezi - Makwaya
Makamba ashiriki mkutano wa 20 wa Mawaziri wa Mambo ya Nje