Aliyekuwa Kiungo wa Hispania Cesc Fabregas amekiri mahaba ya mchezo wa soka yamemzidi kwenye miaka yake ya mwisho na hilo limemsukuma kuhamia kwenye ukocha.
Kiungo huyo wa zamani wa Arsenal, Barcelona na Chelsea sasa ni kocha wa timu ya U-19 ya Como inayoshiriki Ligi Daraja la Pili Italia.
Fabreas mwenye umri wa miaka 36, alisema timu hiyo ya Serie B ni kama njia tu ya kunasa kazi za kunoa timu kubwa zaidi.
Mhispaniola huyo amedai amepata fursa mpya ya kuendelea na soka baada ya kipindi chake cha uchezaji kuvamiwa na majeruhi mfululizo katika siku za mwisho za maisha yake ya soka kama mchezaji.
“Hiki ni kitu kizuri sana kinachotokea kwangu’ alisema na kuongeza.
“Kustaafu baada ya miaka 20 si kitu ambazo nilikitarajia na kuona kama kuna kitu kingine nitakipenda kuzidi soka. Hi itachukua asilimia 88 ya maisha yangu, asilimia 10 kulala na nyingine nitasaidia familia yangu.
Fabregas amepita chini ya makocha mahiri Arsene Wenger, Pep Guardiola, Jose Mourinho na Vicente del Bosque kwa kuwataja kwa uchache.