Kocha Mkuu wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Young Africans Nasreddine Nabi, amesema muda uliosalia kabla ya mchezo dhidi ya Simba SC, unatosha kukiandaa vizuri kikosi chake na kuendeleza furaha kwa mashabiki wa klabu hiyo ya Wananchi.

Miamba hiyo ya Soka la Bongo itakutana Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam Jumapili (April 16), saa kumi na moja jioni kwa saa za Afrika Mashariki.

Nabi amesema kwake anauchukulia umuhimu kila mchezo, hivyo tayari ameshaanza màandalizi atakayoyafanya kwa muda mchache uliosalia kabla ya kuikabili Simba SC.

“Nianze kwa kuwapongeza wachezaji wangu kwa kucheza kila mchezo kwa morali ya juu.”

“Katika mchezo huu tutaingia uwanjani tukiwa tunawaheshimu Simba ni timu yenye mabadiliko lakini hatuwezi kuwa na presha hata kidogo.”

“Hatutaingia uwanjani kucheza kwa ubora mkubwa ili tupate ushindi,” amesema Nabi.

Simba SC itakayokuwa mwenyeji wa mchezo wa Jumapili (April 16), imeachwa kwa tofauti ya alama nane dhidi ya Young Africans inayoongoza msimamo wa Ligi Kuu kwa kuwa na alama 68, baada ya kuifunga Kagera Sugar juzi Jumanne (April 11).

Mipango ya Kocha Robrtinho hadharani
Bursting Hot 5 Ushinda Mpaka Mara 6000 ya Dau Lako