Kocha Mkuu wa Young Africans Nasreddine Nabi amesema bado anaendelea kuwaheshimu Mabingwa wa Tanzania Bara Simba SC, licha kuwafunga kwenye mchezo wa mzunguuko wa pili wa Ligi Kuu (Julai 03-2021).

Nabi ametoa msisitizo wa heshima kwa mabingwa hao mara nne mfululizo, akielekea kwenye mchezo wa mwisho wa Ligi Kuu dhidi ya Dodoma Jiji FC utakaochszwa kesho Jumapili (Julai 18), Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.

Baada ya mchezo huo Nabi atakuwa na kazi ya kuendeleza ubabe mbele ya Simba SC kwenye mpambano wa Fainali Kombe la Shirikisho (ASFC), Uwanja wa Lake Tanganyika mkoani Kigoma Julai 25-2021.

Kocha huyo kutoka nchini Tunisia amesema: “Simba nawaheshimu sana, ni timu yenye wachezaji wazuri lakini sio sababu ya mimi kutopata matokeo katika fainali hiyo muhimu kwetu, na ni moja ya mechi ambayo itanifanya kutamba.”

“Japo tumekosa ubingwa lakini afadhali wanayanga walifurahi mechi iliyopita baada ya kumfunga Simba, tusingeshinda ile mechi na Simba bingwa ingewaumiza zaidi sasa tunageukia FA.”

Young Africans ilitinga Fainali ya ASFC kwa kuifunga Biashara United Mara FC bao 1-0, Uwanja wa Alli Hassan Mwinyi mjini Tabora, huku Mabingwa watetezi wa michuano hiyo Simba SC wakipenya hadi Fainali kwa kuibamiza Azam FC bao 1-0, Uwanja wa Majimaji mjini Songea mkoani Ruvuma mwishoni mwa mwezi Juni.

Mkataba wa Monzinzi kusitishwa Azam FC
Kumbe Nabi hatanii, amezungumza na Mayele