Kocha Mkuu wa Young Africans, Nassredine Nabi amesema ataingia na tahadhari kubwa katika mchezo wa hatua ya Robo Fainali ya michuano ya Kombe la Shirikisho (ASFC) dhidi ya Mwadui FC.

Young Africans watakuwa ugenini mjini Shinyanga kwenye uwanja wa CCM Kambarage, wakicheza dhidi ya wenyeji wao leo Jumanne kuanzia mishale ya saa kumi jioni.

Kocha Nabi amesema anawaheshimu Mwadui FC, na amekua akiwahimiza wachezaji wake watakaopata nafasi kwenye mchezo huo, kucheza kwa nidhamu kubwa.

“Naamini utakuwa mchezo mgumu na wenye upinzani, kwani kila timu itakuwa ikiwania nafasi ya kuingia nusu fainali japokuwa wenyeji Mwadui watakuwa nyumbani mbele ya mashabiki wao, hivyo tunapaswa kuwa makini sana ili tuweze kutimiza malengo yetu.”

“Tunapaswa kuongeza umakini hasa sehemu ya ulinzi tusiruhusu bao na nafasi ya ushambuliaji watumie kila nafasi tutakazo pata ili kujihakikishia nafasi ya kutinga hatua ya nusu fainali,” amesema Nabi.

Mshindi wa mchezo wa leo kati ya Mwadui FC dhidi ya Young Africans atacheza dhidi ya Biashara United kwenye hatua ya Nusu Fainali, ambayo itaunguruma mwezi ujao.

Azam Media kidume Ligi Kuu
Watu wasiojulikana wafukua kaburi, maiti yanyofolewa utupu