Mahakama ya Wilaya Dodoma imempandisha kizimbani mtuhumiwa Onesmo Machibya maarufu kama ‘Nabii Tito’, kwa kosa la kutaka kujiua kwa kujichana chana na wembe.
Shitaka hilo limesomwa na wakili wa Serikali Salome Magesa mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo, James Karayemaha.
Ambapo amesema ‘Nabii Tito’ alitaka kujiua kwa kutumia wembe alijijeruhi kwenye baadhi ya maeneo ya mwili wake wakati akikamatwa na polisi na kwamba ametenda kosa hilo kinyume na kifungu namba 217 na kanuni zake.
Hata hivyo mshtakiwa huyo alipoulizwa na Hakimu amesema alichukua uamuzi huo baada ya kusikia sauti ikisema ajikate na wembe nakudai alitekeleza alichokisikia .
-
Nabii Tito aanza kushughulikiwa
-
Rais Magufuli akutana na Dkt. Slaa Ikulu, wateta
-
Viongozi wa NASA walalama Serikali kuwanyang’anya walinzi
Hakimu huyo amesema kutokana na alichokisikia kutoka kwa Nabii Tito anachukulia kuwa si kweli kuwa ametenda kosa hilo na kuhoji upande wa mashtaka kuhusu upelelezi wa kesi hiyo kama umekamilika.
Hivyo kwa mujibu wa kifungu cha sheria 148(5) (b) cha sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai sura ya 20 amesema amewasilisha mahakamani kiapo cha kupinga dhamana kwa mshtakiwa chenye sababu saba ambazo hakuziainisha ndani ya Mahakama hiyo.
Kutokana na pingamizi hilo Hakimu Karayemaha amesema mshtakiwa huyo ataendelea kuwa rumande hadi hapo Mahakama itakapoamua kuhusu dhamana yake.